Thursday, April 2, 2009

KILICHO MKIMBIZA DUNGA BONGO


Yule Producer mkali aliyekuwa akifanya kazi na studio za 41 Records...aaitwaye Ambros Nkwabi a.k.a 'Dunga'..amerejea nchini kwao Kenya baada ya miaka mitatu mfululizo kupiga kazi za kufa mtu ndani ya Dar.
Akiongea na KIWA MKALI hivi karibuni Producer huyo ambaye hatasahaulika kwa kazi zake bomba,amesema tayari ameshaanza kufanya pini za ukweli na wasanii wa huko kwao akimshirikisha kaka yake aliyemtaja kwa jina la Shakii.Habari hizo zimekuja huku kukiwa na taarifa zilizozagaa jijini kuwa..kilichomkimbiza producer huyo ni kuexpire kwa kibali chake cha kufanyia kazi Bongo....huku wahusika maswala hayo wakimgomea kumuongezea muda mwingine.